Hizi Ndio Dalili, Madhara Na Vyanzo Vya Ugonjwa Wa Amoeba
Huu ni ugonjwa wa maambukizi ya tumboni, yanayosababishwa na bakteria anayejulikana kama Entamoeba Histolytica. Watu wengi wanaugua magonjwa ya tumbo lakini wachache wanaofahamu kuhusu ugonjwa wa amoeba kutokana na uchafu wa mazingira, vyombo vya nyumbani ambao huenezwa kupitia bakteria huyu.
Vimelea wanaoenezwa na bakteria huyu humsababishia mtu kuhara haja ambayo huonekana ina kamasi.
NUKUU: Maambukizi haya mara nyingi hutokana na ulaji wa matunda bila kuyaosha au kutokunawa mikono baada ya kutoka chooni, kula chakula bila kunawa mikono na kunywa maji bila kuyachemsha.
Mgonjwa hupata maambukizi baada ya kunywa au kula kitu kilichochanganyikana na Entamoeba Histolytica ambao hukimbilia kwenye utumbo mdogo ambako huzaliana. Wakiwa wengi huenda kwenye utumbo mkubwa na kuanza kushambulia mwili.
Wadudu hawa wakikua huishi kwenye kinyesi cha binadamu kisha hutolewa kwa njia ya haja kubwa na kuishi katika ardhi kwa muda wa wiki 4, kipindi ambacho huwa na uwezo wa kusababisha maambukizi kwa yeyote atakaye kutana nao. Wanaweza kusambazwa kwa kutokunawa mikono vizuri baada ya kujisaidia, kusambazwa na inzi, kusafisha vyombo kwa maji yasiyo salama, au kushikana mikono na mtu mwenye bakteria hao.
Inasemekana kuwa, kati ya watu milioni 40 mpaka 50 duniani kote wanasemwa kuugua ugonjwa huu ambao husababisha vifo 100,000 kila mwaka. Mara nyingi waathirika wengi huwa hawafahamu kama wanaugua maradhi haya, hivyo kuchelewa kupata matibabu stahiki.
Je, Ni Nani Walio Katika Hatari Zaidi?
Jamii inayoishi katika mazingira yasiyokuwa na maji salama ipo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya amoeba kwani huchota maji kutoka kwenye mito kwa matumizi ya nyumbani bila kujali kwamba ya yanakidhi vigezo vya ki afya.
Vyombo vinapaswa kufutwa kwa kitambaa safi mara tu vinapomaliza kuoshwa. Chakula kitakachochelewa kuliwa kinapaswa kufunikwa ili kuepusha inzi kutua kabla hakijatumika na kuacha bakteria wanaoeneza maradhi haya.
Watu wengine wanaopaswa kuwa makini zaidi ni wale wasionawa mikono baada ya kutoka kujisaidia au wanaobanwa na haja sehemu ambazo hazina huduma ya vyoo na wanaotumia vyoo vya umma ama wasafiri.
Je, Nini Dalili Za Ugonjwa Huu?
Kwa kawaida mtu mwenye ugonjwa wa amoeba hukumbwa na dalili nyingi kama ifuatavyo hapo chini:
- Kuhara
- Tumbo kujaa gesi
- Tumbo kuuma
- Uchovu wa mwili, Kupoteza uzito.
- Maumivu ya kichwa
- Kichefuchefu na kutapika
- Homa, na kutonusa vizuri harufu ya chakula na kutohisi ladha ya chakula
- Tumbo kunyonga na kupata choo kisichoisha
- Kupata choo kilichochanganyikana na makamasi na aendapo chooni, mara nyingi huishiwa nguvu na kushindwa kutembea.
NUKUU: Lakini wagonjwa wengine wanaweza wakapata maambukizi haya ya bakteria hawa lakini wasipate dalili zozote, hivyo yafaa sana kupima choo ili kuhakiki na kuweza kupata matibabu.
Je, Nini Madhara Ya Ugonjwa Huu?
Madhara ya amoeba kwa kawaida huwa kama ifuatavyo:
- Kupungukiwa maji mwilini kutokana na kuharisha
- Kupungukiwa madini muhimu na hivyo kuwa katika hatari ya kupoteza maisha,
- Kuhara damu kupindukia,
- Kutapika au kusikia kizunguzungu,
- Kukosa hamu ya kula na kupata homa kali,
- Utumbo kujikunja,
- Kupata vidonda kutokana na kutoboka kwa utumbo baada ya kushambuliwa na bakteria wengi.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James & Ferdinand Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo haya ya amoeba. Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!
Comments
Post a Comment