Haya Ndio Mambo 6 Yanayofanya Mirija Ya Uzazi Kuziba
Hali ya kujaa maji kwa mirija ya uzazi ya wanawake huitwa kitaalamu, “hydrosalpinx”. Ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo yamekaa muda mrefu bila kutibiwa, kama vile kisonono, pangusa, malengelenge, nk, ambayo kwa ujumla tunaweza kuita maambukizi katika via vya uzazi yaani PID (pelvic inflammatory disease), bila shaka tutayazungumzia baadaye katika makala zinazofuata kwa kuchanganua ugonjwa mmoja baada ya mwingine na tutaona madhara yake na dalili zake pia. Mara nyingi matatizo haya husababisha tatizo la ugumba na maumivu ya kiuno. NUKUU: Mirija ya uzazi hujishikiza upande wa kulia na kushoto mwa tumbo la uzazi, nayo hupitisha mayai kila mwezi kutoka kwenye ovari ama kifuko cha yai, kwenda kwenye mji wa uzazi. Urutubishaji wa yai la uzazi hutokea katika mirija hii. Je, Nini Chanzo Cha Mirija Ya Mayai Kuziba? Mara nyingi mirija ya uzazi kuziba hutokana na magonjwa mengi nayo huwa kama ifuatayo ; Maambukizi katika via vya uzazi ...