Unaweza Kuyashinda Magonjwa Na Dhambi Kupitia Nguvu Za Mungu
Amini Sana Nguvu Za Mungu Hebu tufungue kitabu cha Yoshua, sura ya 11. Miaka iliyopita, mara nyingi nimekuwa nikijifunza kuhusu watu wa Israeli na jinsi gani walivyoingia katika nchi ya Kanaani. Niliona usambamba wa watu wa Mungu katika siku hizi za mwisho na kuingia kwao katika Kanaani ya Mbinguni. Nilijifunza kuachiliwa kwao kutoka utumwani Misri na kuchelewa nyikani. Niliona ulinganifu wa kutolewa kwa Watu wa Mungu kutoka Babeli na kuchelewa kwao nyikani. Niliona uzoefu wa Waisraeli wa kupanda na kushuka na wangapi kati yao waliokufa nyikani. Kisha nimejifunza jinsi walivyopita katika mto Yordani na pia njia yao karibu na Edomu, ambayo tena ilikuwa hadithi ya kuvutia. Ningependa kuendeleza hadithi ambayo kwa sehemu fulani hatujazingatia sana, lakini ambayo inatuhusu sisi leo, na hiyo ndiyo sehemu inayopatikana katika kitabu cha Yoshua. Sura chache za kwanza zinahusu zaidi ushindi wa mji mkuu ambao ulikuwa Yeriko. Kisha hadithi inakwenda kwenye ushindi wa Ai, kipind...