Posts

Showing posts from June, 2024

Mambo 6 Yanayomfanya Mwanamke Kuhisi Maumivu Ya Tumbo Wakati Wa Hedhi Au Baada Ya Kutoka Hedhini

Image
Wanawake wengi huhisi maumivu ya tumbo kabla au wanapokuwa hedhini. Lakini inaweza pia mwanamke akahisi maumivu ya tumbo anapokuwa hedhini. Maumivu haya mara nyingi huwa sio makali sana. Hata hivyo, ni muhimu kwamba unayafuatilia, hasa ikiwa kama yanakaa kwa muda mrefu. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi inaweza kuwa ni dalili ya magonjwa mbalimbali. Endelea kusoma Makala hii ujifunze dalili, visababishi, Pamoja na matibabu ya kukosa hedhi au kutokwa na damu ya hedhi nyingi kwa muda mrefu. Je, Nini Visababishi Vyake? Wakati mwingine maumivu ya tumbo baada ya hedhi huwa sio makali mno. Lakini kama una maumivu makali endelevu yanayodumu muda mrefu kuliko mzunguko wako wa hedhi, inaweza kuwa ishara kwamba una magonjwa kwenye tumbo lako la uzazi(uterus). Hapa nitakuelekeza visababishi vya maumivu ya tumbo unapotoka hedhini: 1.      Endometriosis Endometriosis ni ugonjwa ambao hutoea pale seli zinazofanana na ukuta laini wa mji wa mimba(uterus) zinapoota nje ya mji wa mimba...

Fahamu Chakula Bora Kwa Uzazi Wa Mwanaume

Image
Kwanza napenda kuwapongeza wale wote ambao huwaandaa vijana wa kiume kuwa wababa bora kwa kuwapa mafunzo stahiki. Ili kiwanda cha mbegu kifanye kazi kwa ubora, kinahitaji mlo wenye virutubisho vya kutosha. Kula mlo wenye afya na kufanya mazoezi ya kutosha kunasaidia kuweka mbegu za kiume katika hali nzuri. Vipo vyakula muhimu sana ambavyo baba mtarajiwa anapaswa kuvipata. Navyo ni hi vifuatavyo:- 1. Matunda. 2. Mbogamboga. Mboga lishe ni muhimu sana kwa baba anayehitaji mtoto. Mboga mchanganyiko zisizopungua saba. Mfano, michicha, mnafu, tembele, bamia, majani ya maboga, majani ya kunde, mlenda. zote hizi zipikwe pamoja. 3. Nafaka zote. Viazi vitamu viliwe sana, mahindi ya kuchemsha na ndevu zake pamoja na muhogo hasa muhogo mbichi. 4. Vyakula vya protini ni muhimu sana. Vyakula hivi visikose angalau mara mbili kwa wiki. 5. Vyakula vya maziwa. Vyakula hivi ni kama maziwa fresh, mtindi na jibini, kwa sababu vina mafuta ambayo ni muhimu katika kiwanda cha kuzarishia mbeg...

Fahamu Vyakula Ambavyo Mama Hapaswi Kula Wakati Wa Ujauzito

Image
Neno la Mungu linathibitisha kuwa watoto ni Baraka kutoka kwa Mungu. Mwanzo 1:28. “Mungu akawabarikia,  Mungu akawaambia,  Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya Nchi” Kwahiyo ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili angavu ni lazima apate lishe bora akiwa tumboni mwa mama yake. Vyakula Bora Kwa Ufupi 1. Vyakula vya nafaka na wanga –kwa ajili ya ukuaji wa mtoto. 2. Samaki na nyama-kujenga mwili wa mtoto hasa katika miezi ya 4-9. 3. Vyakula vya mafuta – kwa ujengaji wa seli za mwili. 4. Mbogamboga-kuimarisha mwili na akili ya mtoto. 5. Maji- husaidia mmen’genyo na unyonyaji wa chakula, huzuia choo kigumu, mwili kuvimba na UTI.  Makande Lishe Ni chakula chenye mchanganyiko wanafaka zisizopungua saba pamoja na viungo mbali mbali. Mchanganyiko wake ni kama ifuatavyo: - NAFAKA. 1.      Njugu mawe 2.      Ma...

Mambo 4 Yanayosababisha Kutokwa Na Uchafu Ukeni Wenye Rangi Ya Kahawia

Image
  Hauko kwenye kipindi chako cha hedhi, lakini unaona rangi kidogo kwenye chupi yako. Je, hiyo ni damu ya hedhi? Je, ni uchafu ukeni? Je, ni uchafu pamoja na damu? Je, Kutokwa Na Uchafu Wa Kahawia Ni Kawaida? Wakati damu inapochanganyikana na ute ute ukeni, matokeo yake ni kutokwa uchafu wenye rangi ya kahawia. Wakati mwingine, hii ni ishara tu kwamba kipindi chako kimefika mwisho. "Uchafu wa kahawia wa kawaida hutokea mwishoni mwa mzunguko wako wa hedhi," "Kunaposalia damu kidogo nyuma wakati kipindi cha hedhi kinapoelekea kukoma, mara nyingi mwili huivundisha na bakteria na hivyo hushindwa kutoka." Wakati mwingine, ingawa, baadhi ya uchafu huo huonekana nje ukeni mwako au kwenye nguo yako ya ndani, inapoelekea mwisho wa kipindi chako cha hedhi, au hata siku moja au mbili baada ya kumaliza. Lakini kuna sababu zingine zinazopelekea kutokwa na damu yenye rangi ya kahawia, nazo ni pamoja na: Mabadiliko Yanayohusiana Na Kukoma Kwa Hedhi Unapokuwa katika umri wa kuk...

Fahamu Sababu Zinazomfanya Mwanamke Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa?

Image
Viwango vya wanawake vya hamu ya tendo la ndoa hupungua kadiri wanavyozidi kukua. Ni kawaida viwango vya juu na vya chini kutokea pamoja katika mwanzo au mwisho wa mahusiano. Au viwango hivi vinaweza kutokea kwa mabadiliko makubwa ya maisha kama vile ujauzito, kukoma hedhi au ugonjwa. Dawa zingine zinazotumiwa kwa ajili ya kutibu magonjwa fulani zinazoathiri hisia pia zinaweza kusababisha kushuka kwa hamu ya tedno la ndoa kwa mwanamke. Ikiwa kama hali ya kukosa hamu ya tendo la ndoa inaendelea au inatoweka tena inarudia, na kusababisha shida zako kibinafsi, basi ongea na mtaalamu wako wa afya. Unaweza kuwa na ugonjwa unaoweza kutibika unaoitwa ugonjwa wa kukosa hamu au hisia ya tendo la ndoa. Je, Dalili Zake Ni Nini? Na hata kama hamu yako ya tendo la ndoa iko chini sana kuliko ilivyokuwa hapo awali, bado uhusiano wako unaweza kuwa na nguvu. Nipende kuema hivi: Hakuna kiwango kinachoweza kufafanua upungufu wa hisia au hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke. Ni hali inayotofautiana. Dal...

Fahamu Madhara Yanayotokana Na Ugonjwa Wa PID Wa Muda Mrefu

Image
Ugonjwa wa PID usipopata tiba yake unaweza kusababisha matatizo makubwa ya muda mrefu kwa mgonjwa. Matatizo haya huwa kama ifuatavyo: Ugumba: Mwanamke mmoja kati ya 10 wenye PID hushindwa kuwa na uwezo wa kupata mimba na hivyo kuwa mgumba. PID inaweza kusababisha makovu kwenye mirija ya uzazi. Makovu haya yanaweza kuiziba mirija na kuzuia yai kushindwa kurutubishwa. Mimba Kutunga Nje Ya Uzazi: Kovu kutokana na PID pia linaweza kuzuia yai lililorutubishwa kushindwa kutoka kwenye mrija wa uzazi na kuhamia kwenye mfuko wa uzazi. Badala yake, linaweza kuanza kukua huku likiwa ndani ya mrija wa uzazi. Mrija unaweza kupasuka na kusababisha damu inayohatarisha maisha ndani ya tumbo la uzazi na kwenye nyonga. Upasuaji wa dharura unaweza kuhitajika ikiwa mimba nje ya tumbo la uzazi haitatambuliwa mapema.   Maumivu Ya Nyonga Ya Muda Mrefu: PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga ya muda mrefu ambayo hudumu Zaidi ya miezi 6. Je, Nani Yuko Kwenye Hatari Ya Ugonjwa Wa PID? PID inaweza k...

Fahamu Mambo 3 Yanayopelekea Kuvimba Kwa Shingo Ya Kizazi

Image
Kuvimba kwa shingo ya kizazi kitaalamu tunaita, “Cervicitis” , nayo huwa ni sehemu nyembembe inayokuwa chini mwishoni mwa tumbo la uzazi ambayo hufunguka ndani kwenye uke. Dalili za kuvimba kwa shingo ya kizazi ni pamoja na kutokwa na damu ya hedhi kwa kujirudia mara mbili ndani ya mwezi mmoja, kuhisi maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa, na kutokwa na uchafu ukeni. Hata hivyo, pia inawezekana kupatwa na hali ya kuvimba kwa shingo ya kizazi na kushindwa kuona dalili au ishara zozote. Mara nyingi, kuvimba kwa shingo ya kizazi kunaweza kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, kama vile pangusa au kisonono. Uvimbe wa shingo ya kizazi unaweza kutokana na magonjwa ya siyo ambukiza pia. Matibabu ya ugonjwa huu huhusika na kutiba uvimbe wa shingo ya kizazi. Mara nyingi, kuvimba kwa shingo ya kizazi huwa hauonyeshi dalili, na unaweza kujifunza tu ugonjwa baada ya kupata vipimo. Ikiwa kama una dalili, basi zinaweza kuwa pamoja na hizi zifuatazo:  Kutokwa na uchafu mwingi usio wa ...

Fahamu Sifa Za Nabii Wa Kweli

Image
1.  Nabii wa Kweli Hapendi Kujiita “nabii”! Wale ambao wamebahatika kupata karama ya unabii huona kuwa ni vibaya kujiita jina hilo kwa sababu hupenda kumtukuza Mungu na sio kujitukuza wao wenyewe. Yohana Mbatizaji alikuwa nabii mkubwa kuliko manabii wote kama Yesu alivyosema: Luka 7:26-28 “Lakini, mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambia, na aliye zaidi ya nabii. 27 Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako. 28 Nami nawaambia, Katika wale waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana; lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye.” Hivyo, kulingana na Yesu, Yohana Mbatizaji alikuwa nabii, tena ni zaidi ya nabii. Lakini Yohana Mbatizaji alipoulizwa wewe u nani? Hakujiita kwamba “mimi ni nabii”: Yohana 1:19-21 “Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? 20 Naye alikiri, wala hakukana; ali...